Spijo, Lineo, Martha, Babalwa, Chipo and Mwaise wote wapo njia panda kuhusu mapenzi na mahusiano – ni aina ya matatizo yale yale ambayo yanaweza pata wewe, marafiki zako au rika lako.
Ikiwa ni kuwa kwenye mahusiano na mtu aliye kuzidi umri, mahusiano yasiyo na afya, kufanya ngono bila kondomu, kuwa na uwezo wa kukataa kufanya ngono, njia mbali mbali za uzazi wa mpango na kuweka wazi kuhusu hali yako ya virusi vya ukimwi – haya ni maamuzi makubwa.
Kupitia wahusika wa stori hii unaweza kupata maelezo muhimu katika kila mada, fikiria kuhusu hali zao, na utengeneze mwendelezo wa vile stori itakavyoishia.



